Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2015
Picha
Unaweza Kuwa Vile Unavyotaka Uamuzi Ni Wako Mara nyingi tumekuwa tukitamani kuwa watu wa aina fulani. Wakati mwingine tumetamani kuwa kama baadhi ya watu wenye mafanikio ambao wanatuvutia sana.  Lakini wengi wetu tunaishia kutamani tu bila kufikia pale tunapokusudia. Mara kwa mara tumeaminishwa kuwa watu wanaofikia mafanikio wamezaliwa na bahati, au wengi hutumia usemi wa Kiswahili kuwa “maji hufuata mkondo”. Wakiwa na maana kuwa kuna baadhi ya watu au familia ambazo wamejaliwa kuwa na mafanikio na wengine hawawezi kwakua hawana bahati hiyo. Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu anaweza kufikia kiwango chochote kile cha mafanikio kama akiamua. Kuna baadhi ya kanuni ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kufikia popote unapohitaji bila kujali rangi, kimo, kabila, ukoo wala taifa. Kama ambavyo ukifuata kanuni za kushindwa basi lazima utafikia kushindwa bila kujalisha wewe ni nani na unatokea wapi? Katika kila kiwango unachotaka kufikia, ni vizuri kufahamu kanuni na sheria za k...
Picha
Mambo Nane(8) Yatakayokufanya Uwe Na Fikra Chanya Kila Wakati Ili Uweze Kufikia Mafanikio Habari ndugu msomaji. Leo ningependa tuangalie namna ambavyo unaweza kujijenga na kuwa na fikra chanya kila wakati bila kujali watu wanaokuzunguka au matukio ambayo yametokea na kukuvunja moyo. Siri ya kuwa na mafanikio katika kila unalolifanya ni kuwa na fikra chanya. Ukishakuwa na fikra hasi tu, basi hata kukamilisha matamanio yako itakuwa ngumu. Ni dhahiri kuwa vile tunavyoviona nje vilianzia ndani yetu. Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana kujenga fikra chanya ili kuleta matokeo mazuri ya nje/katika ulimwengu wa mwili.  Tutaangalia baadhi ya vitu vitakavyotusaidia kutujengea fikra chanya na kama utakua na baadhi ya sababu ambazo unahisi kwako ni muhimu katika kukuongezea fikra chanya basi utaongezea na uweke katika karatasi ili kila ukiamka uzipitie, ili hali yoyote ile mbaya inapokukumba ukumbuke kuwa kuna mahala unaweza kusoma na ukarudi katika hali yako ya kawaida. 1.  Kuamka ...