HADITHI YA MWIZI
HADITHI YA MWIZI Habari ndugu msomaji wa blog ya “ boreshamaisha ”. Inawezekana kichwa cha makala hii kimekushitua kidogo. Leo nimetamani sana tujifunze kitu kwa kupitia wezi. Siku moja nikiwa sokoni sehemu wanapouza nguo za mitumba dada mmoja aliyekua akichagua nguo aliibiwa simu. Baada ya mwizi kuchukua simu tu, dada yule alishituka na kupiga kelele za mwizi na watu wakaanza kumfukuza mwizi yule kwa hasira huku kila mmoja akijaribu kuokota silaha iliyopo karibu ili amrushie mwizi yule. Lakini cha ajabu ni kwamba mwizi aliweza kuwatoroka watu wote na kupotea vichochoroni. Naomba uelewe kuwa nia yangu sio kumsifia mwizi kwa kile alichokifanya lakini natamani ujifunze kitu kutoka kwa mwizi huyu. Kwanza mwizi huyu alijipanga tangu muda mrefu. Yaani aliisoma picha yote ya namna wizi wake utakavyokwenda mpaka atakapofanikiwa. Pili mwizi huyu alikua na target. Alifahamu tokea mwanzo ni nini alikitaka kutoka kwa nani na akajipanga kukipata. Nadhani mwizi alitumia muda mwin...