Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2017

Huyu Ndiye Mtu Anayeweza Kukusaidia Kutatua Changamoto Unazozipitia.

Picha
Huyu Ndiye Mtu Anayeweza Kukusaidia Kutatua Changamoto Unazozipitia. Mara nyingi binadamu tumekuwa tukilalamika kuhusu ugumu wa maisha na changamoto kuzidi kuongezeka kadiri siku zinavyozidi kwenda. Katika jamii zetu kuomba msaada ni jambo jema kabisa lakini tunachozingatia ni wapi au kwa mtu wa aina gani tunaomba msaada. Kwa wale wenye imani katika dini kila mmoja na dini yake huomba ili aweze kupata unafuu juu ya changamoto zinazomkabili. Lakini hii haimaanishi kuwa changamoto zinakwisha, ukivuka changamoto moja bado inakuja nyingine na nyingine hivyo hivyo, ilimradi maisha hayaishi changamoto. Na hii hutokea kwa watu wenye vipato vikubwa na vidogo, rika tofauti tofauti kwa ufupi kila mmoja bila kujali hadhi,muonekano au uwezo wake alionao changamoto humkabili. Wakati huu huwa mgumu lakini ugumu huu hutegemea aina ya mtu aliyepata changamoto. Kuna wengine wanaweza kupata changamoto ndogo na kuwa na uwezo mkubwa wa kuzihimili lakini wengine wakawa na changamoto ndogo ...