Unaweza Kuwa Vile Unavyotaka Uamuzi Ni Wako Mara nyingi tumekuwa tukitamani kuwa watu wa aina fulani. Wakati mwingine tumetamani kuwa kama baadhi ya watu wenye mafanikio ambao wanatuvutia sana. Lakini wengi wetu tunaishia kutamani tu bila kufikia pale tunapokusudia. Mara kwa mara tumeaminishwa kuwa watu wanaofikia mafanikio wamezaliwa na bahati, au wengi hutumia usemi wa Kiswahili kuwa “maji hufuata mkondo”. Wakiwa na maana kuwa kuna baadhi ya watu au familia ambazo wamejaliwa kuwa na mafanikio na wengine hawawezi kwakua hawana bahati hiyo. Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu anaweza kufikia kiwango chochote kile cha mafanikio kama akiamua. Kuna baadhi ya kanuni ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kufikia popote unapohitaji bila kujali rangi, kimo, kabila, ukoo wala taifa. Kama ambavyo ukifuata kanuni za kushindwa basi lazima utafikia kushindwa bila kujalisha wewe ni nani na unatokea wapi? Katika kila kiwango unachotaka kufikia, ni vizuri kufahamu kanuni na sheria za k...